Ihefu yakutana na nmpapaso wa Ruvu

Comments · 91 Views

Ruvu Shooting imeanza vyema msimu huu kwenye ligi baada ya kuichapa Ihefu bao 1-0 mchezo uliopigwa leo Agosti 15, kwenye uwanja Highland Estate Mbarali.

Mbeya. Pamoja na msako walioufanya Ihefu kwa mashambulizi mfululizo lakini wamejikuta wakianza vibaya baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu NBC msimu huu.

 Ligi Kuu imeanza leo ambapo Ihefu ikicheza mechi ya kwanza na Maafande hao katika uwanja wake wa nyumbani, Highland Estate Mbarali wamejikuta wakiondoka uwanjani vichwa chini.

Bao pekee katika mechi hiyo, lilifungwa na Ally Bilali dakika ya 19 likiwa la kwanza msimu huu na kuweka rekodi ya kufunga dakika za mapema kuliko msimu uliopita ambapo Willy Edgar alifunga dakika ya 49 akiisaidia Mbeya Kwanza kushinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kipindi cha kwanza Ruvu Shooting walionekana kumudu mpira na kuwafanya kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa mbele, ambapo kipindi cha pili Ihefu walikuwa moto kupeleka mashambulizi sana kwa wapinzani.

Timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa, ambapo Ruvu Shooting waliwapumzisha Bilali na Haruna Chanongo na nafasi zao kujazwa na Samson Joseph na Full Zull Maganga.

Kwa upande wa Ihefu iliwatoa Never Tigere na Mwalyanzi na kuwaingiza Papy Tshishimbi na Issah Ngoah na matokeo hayakubadilika chochote, huku Salum Kipaga na Kipa Hussein Masalanga wakifanya kazi kubwa kuipa Ruvu Shooting alama tatu za kwanza msimu huu kwa kuokoa hatari nyingi.

Comments