VITENDO VYA RONALDO BAADA YA MAN UTD KUFUNGWA 4-0 KUMFUKUZISHA OLD TRAFORD...AC MILAN WAJIANDAA KUMCHUKUA...

Comments · 61 Views

Manchester United inatazama uwezekano wa kusitisha mkataba wa Cristiano Ronaldo ikiwa hatobadili tabia yake.

United wanadaiwa kuwa na wasiwasi kuhusu tabia ya Ronaldo na wanaweza kufikiria kusitisha mkataba wake kabla ya kumaliza.

Ronaldo (37) alitoka nje ya uwanja baada ya United kuchapwa 4-0 na Brentford bila kumpa mkono Erik ten Hag.

Ronaldo alionekana akitupa mikono na kuonyesha hasira yake kwa De Gea baada ya kufanya Makosa. Baada ya filimbi ya muda wote Ronaldo alishindwa kuwapigia makofi mashabiki waliosafiri na kurushiana maneno yaliyoonekana na kocha Steve McClaren kabla ya kuondoka haraka uwanjani.

Wakala wake wakala Jorge Mendes amefanya mazungumzo na AC Milan na wapinzani wao Inter lakini vilabu vyote viwili vimesita kumsajili supastaa huyo.

Klabu za Atletico Madrid na Sporting Lisbon bado hazijajitoa kwa asilimia 100 kumsajili Ronaldo.

Comments