Ahmed Ally: Maumivu ni makali sanaa

Comments · 83 Views

Alichoposti msemaji wa Simba Ahmed Ally baada ya kipigo cha 2-1 cha Ngao ya Jamii kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga.

“Hakuna anaeweza kujificha kwa kusema ni kawaida ya mpira, mateso hayapaswi kuwa kawaida

Ukweli ni kwamba tunapitia maumivu makali mnoo, kila mwana Simba leo anaugua kivyake

Poleni sana ndugu zangu hakuna neno la kufuta machungu yenu

Mlichokitegemea sicho mlichopata inaumiza sana, kila nikitazama macho ya Wana Simba naona uchungu na maumivu yaliyopitiliza, kiukweli mnateseka ndugu zangu.

Tumeshapoteza, tutulie tuone tunaingiaje msimu mpya, Sio rahisi kusahau lakini tunapaswa kujisahaulisha maana ligi inaanza wiki ijayo ni muhimu zaidi kuanza vizuri

Panapovuja pameonekana tuwaachie wahusika wafanye maamuzi sahihi

Comments