Chelsea, Spurs ‘ngoma droo’ makocha wao wakitunishiana msuli

Comments · 67 Views

Timu ya Chelsea imelazimishwa sare ya magoli 2-2 ikiwa nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, maarufu kama EPL.

Mechi hiyo imepelekea mabosi wa timu hizo, Thomas Tuchel (Chelsea) na Antonio Conte kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu baada ya ‘kutoleana povu’.

Makocha hao ambao hawaelewani, walisogeleana’ pua kwa pua’ wakitunishiana msuli’

Baadae walitenganishwa na refa wa mchezo huo Antonio Taylor na kuwapa kadi nyekundu.

Kwa matokeo hayo, timu hizo zimefikisha pointi 4 kila moja katika michezo miwili.

 

Comments