Simba yatangaza mkataba MNONO wa TSH Bilioni 26.1

August 1, 2022

“Zile zama za kuwa na mkataba sare sare maua zimepita. Kwa miaka ya hivi karibuni Simba tumewekeza vya kutosha ili kuhakikisha brand yetu inakua,”- Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.

“Process ya mdhamini mpya tulianza tangu mwaka jana. Tumepokea ofa nyingi za kutaka kuwa main sponsor, lakini M-Bet ndio wamekidhi vigezo vyetu vyote,”

CEO wa Simba, Barbara Gonzalez.

“Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania.”- Barbara

“Hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na senior team pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake,”- CEO

Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi ametaja mchanganuo wa udhamini mpya wa Klabu ya Simba:

Mwaka wa kwanza – Bil 4.670
Mwaka wa pili – Bil 4.925
Mwaka wa tatu – Bil 5.205
Mwaka wa nne – Bil 5.514
Mwaka wa tano – Bil 5.853
Jumla ni Bilioni 26, Milioni 168 na Tsh. 5,000.

47 Views